You are currently viewing TRIO MIO KUTUMBUIZA KWENYE KONGAMANO LA AZIMIO LA UMOJA IJUMAA HII

TRIO MIO KUTUMBUIZA KWENYE KONGAMANO LA AZIMIO LA UMOJA IJUMAA HII

Rapa anayekuja kwa kasi nchini Trio Mio ametajwa kuwamiongoni mwa wasanii watakaotumbuiza kwenye kongamano la  Azimio la Umoja linalotarajiwa kufanyika katika uwanja wa kimataifa wa moi kasarani Ijumaa hii, Disemba 10.

Rapa huyo ambaye ni mchanga kwenye tasnia ya muziki nchini amethibitisha hilo kupitia video iliyochapishwa kwenye ukurasa rasmi wa twitter wa kinara wa ODM Raila Odinga.

Katika video hiyo fupi, rapA huyo ambaye bado anasoma shule ya upili, amewataka Wakenya kujitokeza  kwa wingi kwenye kongamano hilo, ili kusikiliza kile ambacho kiongozi huyo wa ODM atakizungumza.

Hata hivyo takriban wajumbe na wafuasi 60,000 watatajiwa kuhudhuria hafla hiyo katika Uwanja wa Kimataifa wa Moi, Kasarani.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke