You are currently viewing Tunisia yatupwa nje ya michuano ya Kombe la Dunia 2022

Tunisia yatupwa nje ya michuano ya Kombe la Dunia 2022

Timu ya Taifa ya Tunisia imetupwa nje ya michuano ya Kombe la Dunia licha ya kupata ushindi wa 1-0 mbele ya mabingwa watetezi wa michuano hiyo timu ya Taifa ya Ufaransa kwenye mchezo wa mwisho wa kundi D

Alama 4 za Tunisia hazikutosha kuwavusha katika hatua inayofuata ya michuano hiyo baada ya Australia kuibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Denmark katika mchezo mwingine wa kundi hilo na kuzima ndoto za Waafrika kushuhudia wawakilishi wao wengine wakifuzu hatua ya 16 Bora ya michuano hiyo mikubwa zaidi ya mchezo wa kandanda Duniani baada ya Senegal kutangulia katika hatua hiyo hapo Novemba 30.

Matokeo hayo yameifanya Tunisia kumaliza katika nafasi ya tatu kwenye kundi hilo nyuma ya Australia na Ufaransa aliyeongoza na alama 6.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke