Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa mtandao wa Twitter, Elon Musk ametangaza kwamba, Twitter inatarajia kuongeza kipengele kipya ndani ya jukwaa hilo kitakacho onesha idadi ya watu waliopita na kuona chapisho (tweet) la mtumiaji.
Musk ambaye tangu aununue mtandao huo Oktoba mwaka huu kwa dola bilioni 44, kasi yake ya kuweka vipengele vipya katika jukwaa hilo inakosolewa vikali.
Kipengele hicho, ambacho tayari kipo kwa ajili ya video, kitaonyesha nii kiasi gani Twitter iko hai kuliko inavyoweza kuonekana,” Musk aliandika, akifafanua kwamba “Zaidi ya asilimia 90 ya watumiaji wa Twitter wanasoma, lakini hawa- tweet, kujibu au kuonesha hisia (like) kama matendo ambayo yako wazi.”