Mtandao wa Twitter umeanza majaribio ya kuweka matangazo katika sehemu ya Replies/comments.
Ni style mpya ya kuonyesha matangazo katikati ya comments/replies. Inaonekana matangazo yataonekana sana katika Tweets za watu maarufu na akaunti ambazo zina watu wengi wanaoshiriki katika comments.
Bado haijaonekana kama mwenye akaunti atafaidika na matangazo ambayo yataonekana katika Replies za Tweets zake. Tayari imeanza kwa watumiaji wa App ya Beta katika iOS na Android.