Twitter imefanya mabadiliko katika sehemu ya search. Sasa hivi unaweza kuona thamani ya hisa na cryptos katika sehemu ya Search.
Mfano ukitaka kutazama thamani ya hisa za Apple kwa sasa unaweza kuandika $aapl au $AAPL na utaona thamani ya hisa za Apple kwa ripoti ya siku.
Inaonekana unaweka $ kama ukitaka kuona thamani ya hisa au crypto kwa Dola. Lakini ukiweka alama za ¥ € ¥ £ ₦ bado hauwezi kuona thamani ya hisa na crypto kwa currencies zaidi ya Dola.
Kwa twitter ni idea nzuri kwa sababu mtandao huu unatumika sana na watu wengi kufuatilia trends za Hisa na Cryptocurrencies. Inaonekana imeshirikiana na Robinhood kuweka graphs na bei za hisa na crypto.