You are currently viewing TWITTER YAWEKA UTARATIBU WA KUZUIA KUPOST PICHA YA MTU BILA RUHUSA YAKE
FILE PHOTO: People holding mobile phones are silhouetted against a backdrop projected with the Twitter logo in this illustration picture taken in Warsaw September 27, 2013. REUTERS/Kacper Pempel/File Photo

TWITTER YAWEKA UTARATIBU WA KUZUIA KUPOST PICHA YA MTU BILA RUHUSA YAKE

Twitter imeweka utaratibu mpya wa kuzuia ku-post picha ya mtu bila ruhusa yake. Twitter imesema ni marufuku kutuma au ku-post picha binafsi ya mtu bila ruhusa yake. Ku-tweet picha au video ya mtu ni kosa na inaweza kupelekea kufungiwa akaunti yako. 

Endapo mtu akipost picha ya mtu bila ruhusa yake, mtu huyo anaweza kuripoti picha hiyo na twitter itaifuta na kutoa adhabu kwa mtu aliyepost bila ruhusa. Kiutaratibu kabla ya kupost video ya mtu unatakiwa mpatia Consent Form inayothibitisha huyo mtu amekupa ruhusa.

Kanuni hii ina mapungufu yake, haigusi watu maarufu kwa sababu inaweza kuwa ni habari. Hivyo kama ni picha au video ya mtu maarufu au vyombo binafsi vya habari, hakuna tatizo kupost.

Pia ni marufuku ku-post taarifa za namba za simu za mtu, address yake, majina yake, namba zake za ID, vitambulisho au taarifa ambazo sio zako

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke