App ya Twitter imeweka sehemu mpya ya kurekodi mijadala ya Live-Audio (Twitter Spaces). Wasikilizaji watakuwa na uwezo wa kusikiliza Twitter Space baada ya Live-Audio kuisha.
Twitter imesema itahifadhi file kwa muda wa siku 120, ili kuhakiki kama maudhui yake ni sahihi. Hivyo hata ukifuta, bado file litabaki Twitter ili kusaidia uchunguzi endapo kama itakuwa reported.
Twitter kuweka sehemu ya kurekodi mijadala ya live-audio ni kwa sababu ya kuongeza ushandani na app ya Clubhouse ambayo hivi karibuni iliweka features mpya za Clips na Replay ambazo zinawezesha watumiaji kutunza mazungumzo.