You are currently viewing UCHAGUZI WA CHAMA CHA WASANII UGANDA UMA KUFANYWA JUNI 28

UCHAGUZI WA CHAMA CHA WASANII UGANDA UMA KUFANYWA JUNI 28

Hatimaye Chama cha Wanamuziki Uganda UMA imetangaza tarehe ya kufanyika kwa uchaguzi wa chama hicho baada ya kufutwa kwa upigaji kura Juni 6 mwaka huu kutokana na kukumbwa na dosari.

Katika mkao na wanahabari uma imesema uchaguzi huo utafanyika Juni 28 mwaka huu huko National Theatre garden jijini Kampala ambapo itafanyika kwa mfumo wa kawaida wakupanga foleni kwenye kituo cha kupigia kura.

Kulingana na uma upigaji wa kura katika chama hicho utafanyika  kwenye kituo kimoja hivyo wanachama wake watalazimika kusafari hadi kampala kwa ajili ya kushiriki kwenye uchaguzi huo kwani hawana pesa za kutosha kuandaa uchaguzi katika vituo vingi.

Utakumbuka Uchaguzi wa UMA uliahirisha Juni 6 mara baada ya wafuasi wa King Saha kudai kwamba uchaguzi huo uligubikwa na wizi hadi sasa Kamati ya inayojishughulisha na uchaguzi hajatoa mweelekeo kama uchaguzi utarudiwa ila jambo la kusubiriwa.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke