You are currently viewing Ufaransa yatinga Fainali Kombe la Dunia 2022

Ufaransa yatinga Fainali Kombe la Dunia 2022

Mabingwa watetezi wa michuano ya Kombe la Dunia timu ya taifa ya Ufaransa imefanikiwa kutinga fainali ya michuano hiyo baada ya kuwazaba 2-0 Morocco

Theo Hernandez wa ufaransa alipachika bao la kwanza katika dakika ya 5 ya mchezo huo huku mshambuliaji Randal Kolo Muani akipachika bao la pili na kufunga kitabu cha magoli katika dakika ya 79 ya mchezo na kufuta matumaini ya Morocco kucheza fainali ya kombe la dunia kwa mara ya kwanza.

Morocco ambao ni wawakilishi pekee wa Bara la Afrika waliokuwa wamesalia kwenye michuano hiyo sasa wataisaka nafasi ya tatu kwa kuvaana na Croatia

Ufaransa watajaribu kutetea taji lao mbele ya Argentina kwenye mchezo wa fainali siku ya Jumapili Desemba 18.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke