Mwanamuziki Cindy Sanyu amedai kuwa chama cha wasanii nchini Uganda UMA itashirikiana na makampuni ya kutoa huduma ya mazishi nchini humo kuhakikisha wasanii wanazikwa kwa heshima pindi wanapofariki.
Akizungumza kwenye hafla ya kuwaombea wasanii waliotangulia mbele za haki juzi kati, Cindy amesema wasanii wengi ambao walifariki miaka ya hapo nyuma hawakupokea upendo wa dhati kwenye mazishi yao licha ya kuacha alama kwenye tasnia ya muziki nchini Uganda.
Lakini pia amewashauri wasanii kujenga tabia ya kuweka akiba kama njia moja ya kuondokana na madeni wakati wa majanga.
Miongoni mwa wasanii waliombewa kwenye hafla hiyo ambayo ilihudhuriwa na mastaa mbali mbali ni pamoja na Mowzey Radio, Sera, Martin Angume, Ak-47 na wengine kibao.