Menejimenti ya Mwanamuziki Jose Chameleone kupitia Afisa Uhusiano wake, imetoa maelezo kuhusiana na video ambayo imetoka ikimuonesha mwimbaji huyo maarufu wa nchini Uganda akimpiga mhudumu wa boda boda.
Taarifa hiyo imeeleza kwamba tukio hilo lilitokea November 12, mwaka 2022 ambapo mwendesha boda boda huyo aliichuna kwa pembeni gari ya Jose Chameleone aina ya Range Rover. Taarifa hiyo iliendelea kusema, Chameleone angeweza kupuuzia tukio hilo kama sio maneno ya matusi na vitisho kutoka boda boda huyo.
Tukio linaloonekana ni Jose Chameleone akijaribu kujilinda mwenyewe dhidi ya mwendesha boda boda huyo ambaye alikuwa akimfuata kwa shari. Aidha taarifa ya menejimenti ya Chameleone inakamilika kwa kulaani kitendo hicho.