Uongozi wa Tuzo za Grammy umetaja tarehe mpya ya kufanyika hafla ya ugawaji wa Tuzo hizo kwa mwaka 2022 ambapo sasa itafanyika April 3 katika ukumbi wa MGM Grand Jijini Las Vegas nchini Marekani.
Awali Tuzo hizo za 64 zilipangwa kufanyika January 31 lakini ziliahirishwa kufuatia tishio la kirusi cha Omicron.
Mshereheshaji wa Tuzo za mwaka huu alitajwa kuwa ni mchekeshaji maarufu wa Afrika Kusini, Trevor Noah.