Promota Balaam Barugahara amethibitisha kuwa usalama wa mwanamuziki Eddy Kenzo umeimarishwa baada ya kutishiwa maisha na watu wasiojulikana.
Kwenye mahojiano yake, promota huyo amesema njama ya wanaopanga kumtoa uhai Kenzo haitafaulu kamwe ikizingatiwa kuwa msanii huyo tayari ana walinzi wengi waliojihami na silaha kali za moto.
Baalam ameongeza kuwa njama hiyo inaweza tu kufanikiwa iwapo watesi wake watatumia njia ya uchawi.
“Wale wanaotaka kumuua Kenzo wanaweza tu kufanikiwa kupitia uchawi. Ameimarisha usalama wake na walinzi wenye uzoefu,” Balaam alisema kwenye mahojiano na YouTuber mmoja nchini Uganda.
Mapema wiki hii, Kenzo alifichua kuwa anapokea jumbe za kumtishia maisha ambapo alienda mbali zaidi na kuwataka Waganda kumuombea.