You are currently viewing VANESSA MDEE AZUNGUMZIA ISHU YA KUPATWA NA MSONGO WA MAWAZO BAADA YA KUJIFUNGUA

VANESSA MDEE AZUNGUMZIA ISHU YA KUPATWA NA MSONGO WA MAWAZO BAADA YA KUJIFUNGUA

Staa wa muziki wa Bongofleva, Vanessa Mdee amesema alipatwa na msongo wa mawazo baada ya kujifungua mtoto wake kwanza, Seven.

Kwenye mahojiano na Podcast ya Swahili Nation Vanessa amesema msongo wa mawazo baada ya kujifungua ulimletea madhara licha ya sapoti kubwa anayopata kutoka mchumba wake, Rotimi.

Hitmaker huyo wa ngoma ya “Bambino” amesema kuwa watu wengi hawaelewi huzuni hiyo na labda wanapomwona mtandaoni akiwa na furaha hudhania kuwa ana furaha maishani mwake.

Hata hivyo amewataka wanaume na hata kila mtu katika Jamii kukomesha unyanyapaa dhidi ya afya ya akili kwani kwa sasa anajaribu kupona na ana matumaini mambo yatakuwa sawa.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke