You are currently viewing VDJ JONES AJIBU TUHUMA ZA KUWAIBIWA WASANII ZILIZOIBULIWA NA MSANII PARROTY

VDJ JONES AJIBU TUHUMA ZA KUWAIBIWA WASANII ZILIZOIBULIWA NA MSANII PARROTY

Dj maarufu nchini Vdj Jones amenyosha maelezo kuhusu madai yaliyoibuliwa na Parroty kuwa hajawahi walipa wasanii aliowashirikisha kwenye project zake..

Katika mahojiano na Plug tv Vdj Jones amesema madai hayo hayana msingi wowote kwa kuwa amekuwa akiwalipa wasanii wote aliowashikisha kwenye kazi zake kwa usawa

DJ huyo ameenda mbli zaidi na kusema kwamba ameshangazwa na msanii huyo kumuongelea vibaya mtandaoni ikizingatiwa kuwa amekuwa akimuomba msaada kimuziki.

Bosi huyo wa Superstar Entertainment ameweka wazi tusioyajua kuhusu Parroty kwa kusema kwamba msanii huyo hajawahi walipa wasanii aliowashirikisha kwenye wimbo wake wa Lewa Remix.

Hata hivyo ametoa changamoto kwa wasanii kutia bidii kwenye kazi zao za muziki badala ya kulalamika mtandaoni.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke