You are currently viewing VDJ Jones akiri uhaba wa nyimbo mpya kwenye soko la muziki nchini Kenya

VDJ Jones akiri uhaba wa nyimbo mpya kwenye soko la muziki nchini Kenya

Bosi wa lebo ya Superstar Entertainment VDJ Jones amesikitishwa na maendeleo ya tasnia ya muziki nchini Kenya kwa kusema kwamba kuna uhaba mkubwa wa nyimbo mpya sokoni.

Kupitia video aliyochapisha kwenye mtavndao Facebook VDJ Jones amesema kwa sasa madeejay wanapata ugumu wa kucheza muziki wa Kenya kwa kuwa wasanii hawatoi nyimbo kama kipindi cha nyuma, jambo ambalo liwamepelekea kuwategemea wasanii wa nje ambao wamekuwa wakiachia nyimbo mpya kila mara.

Aidha amesema wasanii wa Kenya wasipotia bidii kwenye kazi zao za muziki huenda wasanii wa mataifa mengine wakateka soko la muziki nchini kwa  kutumbuiza kwenye matamasha mbali mbali ya muziki.

Hata hivyo  ametoa changamoto kwa wasanii wa kenya kuanza kurekodi nyimbo mfululizo bila kupoa badala ya kusubiri wawe vizuri kiuchumi ndio waachie audio pamoja na video kwani mashabiki hawana subira.

Kauli ya VDJ Jones inakuja wakati huu mchekeshaji Eric Omondi anaendelea kuwashinikiza wasaniii waachie nyimbo kwa kuwa wabunifu kwenye suala la kutengeneza matukio yatakayowafanya wazumngumzie kwenye vyombo vya habari.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke