You are currently viewing VDJ JONES AITAKA UDA KUMLIPA EXRAY KWA KUTUMIA WIMBO WAKE “SIPANGWINGWI” KWENYE KAMPEINI ZA KISIASA

VDJ JONES AITAKA UDA KUMLIPA EXRAY KWA KUTUMIA WIMBO WAKE “SIPANGWINGWI” KWENYE KAMPEINI ZA KISIASA

Dj maarufu nchini Vdj Jones ametoa wito kwa chama cha uda kinachoongozwa na Naibu Rais Dakta. William Ruto kumlipa msanii Exray kwa kutumia wimbo wake wa “Sipangwingwi” kwenye kampeni zao za kisiasa.

Kwenye mahojiano na Plug tv, Vdj Jones ambaye pia mwanamuziki amesema ameumizwa sana na kitendo cha wanasiasa kutumia wimbo wa sipangwingwi kujitakia makuu ilhali Exray anaishi maisha ya uchochole mtaani.

Hata hivyo ametaka haki itendeke juu ya suala hilo ila walimwengu kwenye mitandao ya kijamii wameonekana kutofautiana kimawazo na Vdj Jones ambapo wametaka aache ishu ya kutumia jina la Exray kutafutia kiki.

Utakumbuka mapema Exray alifunguka kuwa wimbo wake wa “Sipangwingwi” umempa mafanikio makubwa kwani wimbo umempelekea kumiliki gari.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke