Soshalaiti maarufu mtandaoni Vera Sidika amedaiwa kuwa mjamzito. Tetesi hizo zimeibuka mara baada ya wengi kumuona kwenye mitandao ya kijamii akiwa ameficha tumbo lake mbele ya camera jambo ambalo si kawaida yake.
Lakini pia nguo kubwa (Oversize) ambayo amekuwa akivalia katika siku za hivi karibuni limefanya walimwengu kupigia mstari kuwa mrembo huyo ni mjamzito.
Ikiwa ni kweli Vera Sidika ana ujauzito kwa sasa, basi huyo atakuwa mtoto wa pili kwa staa huyo mwenye umri wa miaka 33 na mchumba wake msanii Brown Mauzo.