Mrembo maarufu nchini Kenya, Vera Sidika amevunja kimya kuhusu madai kuwa ni mjamzito kwa mara ya pili.
Wanamitandao wamekuwa wakidai kuwa mama huyo ni mjamzito kwani amekuwa akificha tumbo lake kila anapoenda.
“Mbona muamini hayo? hii ilikuwa mwaka jana nilipokuwa na mimba ya Asia na nilificha nikiwa nimevalia nguo hii, dah! watu wanaweza kueneza uvumi,” aliandika Vera Sidika Instagram.
Uvumi huo unachukua nafasi baada ya Vera kuweka wazi kuwa amepanga kumpeleka mtoto wake, Asia Brown shuleni ifikapo Januari 2023.