You are currently viewing Vera Sidika atamani kupata mtoto wa kiume

Vera Sidika atamani kupata mtoto wa kiume

Mwanasosholaiti Vera Sidika amesema kuwa anatamani kuwa na mtoto wa kiume siku za mbeleni ili wawe na ukaribu kama wa bintiye Asia Brown na baba yake Brown Mauzo.

Vera amesema kuwa sababu yake ya kutamani kuwa na mtoto wa kiume ni kuwa anauonea wivu urafiki wa karibu ambao Asia na Brown Mauzo wako nao.

“Mwenyenzi Mungu, naombea miujiza katika maisha yangu, natumai huko mbeleni utanipa mtoto wa kiume, nitamringia mume wangu, awacha tu,” alisema Vera anayetamba na ngoma, Popstar.

Vera ambaye hivi karibuni kaachia wimbo wake mpya ‘Popstar’ amejaliwa mtoto mmoja na Msanii wa muziki Kenya, Brown Mauzo baada kuachana na aliyekuwa mpenzi wake, Otile Brown ambaye ni msanii pia.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke