You are currently viewing Vera Sidika athibitisha kuwa mjamzito

Vera Sidika athibitisha kuwa mjamzito

Mrembo maarufu nchini Kenya, Vera Sidika ni mjamzito kwa mara nyingine ikiwa ni siku chache zimepata tangu tetesi  zilipoibuka mtandaoni kuwa amekuwa akificha tumbo lake mbele ya camera.

Kupitia ukurasa wake wa instagram Vera amethibitisha kuwa anatarajia mtoto wake wa pili na mumewe Brown Mauzo huku akieleza ni furaha kwake kupata mtoto mwingine

Mwanamama huyo wa mtoto mmoja amefichua kwamba amekuwa mjamzito kwa takriban miezi saba sasa kwani aligundua ana uja uzito alipokuwa amepanga kuenda nje ya nchi kufanyiwa upasuaji wa kuongeza matiti.

Brown Mauzo kwa upande wake amemshukuru Vera Sidika kwa kuwa mke bora kwake na mama mzuri kwa mtoto wao, Asia Brown.

Hata msanii huyo amemhakikishia kuwa ataendelea kumuonyesha upendo mkubwa huku akikiri kuwa anafurahia hatua nyingine katika ndoa yao.

Utakumbuka wawili hao wamekuwa kwenye ndoa kwa zaidi ya miaka miwili na walibarikiwa na mtoto wao wa kwanza Oktoba mwaka jana.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke