Baada ya kuchafua hali ya hewa siku chache zilizopita, Mrembo Vera Sidika ameachia rasmi wimbo wake mpya kupitia mtandao wa Youtube.
Inawezekana mpaka sasa watu wengi wameamini kilichosemwa na Vera Sidika juu ya kutoa shepu yake, lakini ukweli umejidhihirisha baada ya kuachia wimbo wake mpya, unaokwenda kwa jina la “POPSTAR”.
Wimbo wa Vera Sidika ameuimba kwa miondoko ya Hiphop na baadhi ya comment za Wakenya zimemtaadharisha Diana B kuwa Vera amekuja kumpindua kimuziki.