Mrembo Vera Sidika amekanusha madai ya kufanya upasuaji kuongeza makalio yake kwa kusema kuwa makalio yake ni ya asili.
Katika kikao cha maswali na majibu kwenye mtandao wa Instagram na Mashabiki zake Vera amekiri kuwa athari za dawa za kupangaza uzazi ndio ilichangia ukubwa wa makalio yake.
Mama huyo wa mtoto mmoja amesema alipata unyanyapa mkubwa akiwa shule ya upili mashinani kutokana na watu kumbandika majina ya kukejeli muonekano wa makalio yake lakini alipohamia Nairobi watu walimfanya ajihisi mwenye thamani baada ya kushirikishwa kwenye video ya wimbo wa ‘You Guy’ wa kundi la P-Unit.
Katika hatua nyingine Vera Sidika amesisitiza kuwa matiti yake sio ya asili ambapo ameweka wazi kuwa alifanyiwa upasuaji uliogharimu shillingi millioni 2 za Kenya ili kuongeza ukubwa wake.
Wiki iliyopita Vera Sidika aliteka mitandao ya kijamii baada ya kuposti picha iliyofanyiwa ukarabati wa kupunguza makalio yake ambapo alijitokeza na kudai kuwa alilazimika kufanyiwa upasuaji wa kupunguza makalio kutokana na matatizo ya kiafya lakini ilikuja ikabainika kuwa ilikuwa ni njia ya kutengeneza mazingira ya kuzungumziwa mitandaoni kabla ya ujio wa wimbo wake mpya uitwao Popstar.