You are currently viewing Verckys Kiamuangana Mateta afariki dunia akiwa na umri wa miaka 78

Verckys Kiamuangana Mateta afariki dunia akiwa na umri wa miaka 78

Mwanamuziki mashuhuri kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Verckys Kiamuangana Mateta amefariki dunia huko Kinshasa akiwa na umri wa miaka 78.

Verckys amefariki dunia baada kupatwa na maradhi ya kiharusi miezi kadhaa iliyopita.

Mwanamuziki huyo ambaye alikuwa mkali wa kupuliza Saxaphon, ameacha watoto 32, huku wawili ambao ni Ancy na Daniel wakifuata nyayo zake katika muziki.

Utakumbuka Verckys alitamba miaka ya 70 na 80 kupitia bendi za Ochestra Veve, Lipua Lipua na Kiam. Lakini pia alimiliki studio ya kurekodi muziki iitwayo Edition Veve ambayo bendi nyingi maarufu enzi hizo zikiwemo Lipua Lipua, Les Kamale, Shama Shama, Bella Bella, Kiam, Zaiko Langa Langa zilirekodi nyimbo zao kwake.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke