You are currently viewing VICMASS LUODOLLAR AZUA GUMZO MTANDAONI KWA KUIKATAA SHOW YA LAKI 7 ZA KENYA

VICMASS LUODOLLAR AZUA GUMZO MTANDAONI KWA KUIKATAA SHOW YA LAKI 7 ZA KENYA

Rapa wa michano kwa lafudhi ya Dholuo Vicmass Luo dollar ameibuka na kujinasibu kuwa alilazimika kusitisha onesho lake lenye thamani ya shillingi laki saba za Kenya kwa sababu waandaji wa shoo hiyo waliandika jina lake vibaya kwenye bango la matangazo.

Akipiga stori na Tuko Extra rapa huyo amesema promota wa onesho hilo aliandika jina lake  la Vicmass na s moja jambo ambalo lilimkasirisha na kumpelekea kuchukua maamuzi magumu ya kuikataa show hiyo.

Hitmaker huyo wa “Bank Otuch” ameenda mbali zaidi na kusema kuwa shillingi laki saba ni pesa kidogo kwake ikilinganishwa na jina lake la usanii huku akijigamba kuwa ni heri alale njaa kuhakikisha jina lake linaandikwa vizuri.

Hata hivyo walimwengu kwenye mitandao ya kijamii wameonekana kutofautiana kimawazo na kauli ya rapa huyo wengi wakidai kuwa huenda ana matatizo ya akili kwani mtu timamu hawezi kataa shillingi laki saba za Kenya kisa jina lake limeandikwa vibaya.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke