Msanii kutoka Uganda Victor Kamenyo amezua gumzo mtandaoni mara baada ya video kusambaa ikimuonesha akimshushia kichapo cha mbwa mwanamke mmoja anayedaiwa kuwa ni mpenzi wake.
Video hiyo ambayo inadaiwa kurekodiwa na jirani yake imeibua hisia mseto miongoni mwa watumiaji wa mitandao ya kijamii, wengi wakimtaka msanii huyo achukuliwe hatua kali za kisheria kwa hatua ya kumdhalilisha kijinsia mwanamke huyo.
Victor Kamenyo hata hivyo amekuwa akihusishwa na kashfa nyingi kwenye muziki wake, kwani kuna kipindi alitupwa nje ya nyumba aliokuwa akiishi kwa kukosa kulipa kodi na tangu kipindi hicho amekuwa akisuasua kimuziki.