Video za muziki za msanii nadia mukami zimefutwa kwenye akaunti ya mtandao wa youtube ya msanii huyo.
Ukitembelea kwenye akaunti ya youtube ya nadia mukami hautafanikiwa kuziona nyimbo zake kama maombi, Wangu, Radio Love na Kolo kutokana na kuondolewa na aliyezi-upload.
Sanjari na hilo nyimbo za Nviiri the story teller Pombe sigara na niko sawa zimeondolewa pia kwenye mtandao wa youtube.
Hata hivyo chanzo cha music video za wasanii hao kuondolewa kwenye mtandao wa youtube haijajulikana mpaka sasa.
Ikumbukwe siku ya jana Msanii otile brown alipata pigo kama hilo baada ya video tano za nyimbo zake kuondolewa kwenye mtandao.
|