Video vixen Brenda Otieno amefichua kuwa hakuwahi kulipwa pesa zozote alipotokea kwenye wimbo wa ‘Adhiambo’ wake msanii Bahati pamoja na Prince Indah.
Katika kikao cha Maswali na Majibu na mashabiki wake kwenye mtandao wa instagram, mrembo huyo amefichua kwamba hakuwahi kupokea malipo yeyote aliposhirikisha kwenye wimbo wa Adhiambo akisema kwamba kiasi cha pesa alichoahidiwa kulipwa ni shillingi elfu 10k ambayo haikuwa kiwango chake cha malipo anachowatoza wanamuziki wanaotaka kufanya nae kazi.
Brenda ambaye asili yake anatoka ukanda wa ziwa victoria pia amepuzilia mbali madai yanayosambaa mtandaoni kuwa kuna mtu kwenye video hiyo ya wimbo wa Adhiambo anafadhili mtindo wake wa maisha.
Wimbo wa ‘Adhiambo’ kutoka kwa mzima bahati na prince indah kwa sasa umetazamwa na watu milioni 13 kwenye mtandao wa youtube na ulikuwa gumzo nchini kutokana na watu maarufu walioshiriki katika wimbo huo kama Jaguar, Eric Omondi, Terrence Creatives, Babu Owino na Jalang’o.