Staa wa muziki duniani Rihanna ameweka rekodi kwenye mtandao wa YouTube licha ya kuwa nje ya muziki kwa takribani miaka 6 sasa. Video ya wimbo wake “Diamonds” imefikisha jumla ya views bilioni 2 kwenye mtandao huo.
Ngoma hiyo iliachiwa rasmi Septemba 26, mwaka 2012 na video yake ilipakiwa kwenye mtandao wa YouTube Novemba 9, mwaka 2012.
Diamond ni ngoma kutoka kwenye Album yake ya 7 (Unapologetic) ya mwaka 2012, na iliandikwa na Mwanamama Sia huku ikitayarishwa na Benny Blanco pamoja na Stargate.