You are currently viewing Video ya Fresh Kid “Mazima” yafungiwa Uganda kisa maudhui ya dini

Video ya Fresh Kid “Mazima” yafungiwa Uganda kisa maudhui ya dini

Idara ya upelelezi wa Jinai DCI , imeagiza kusitishwa kwa video ya wimbo wa msanii Fresh Kid “Maziima” kutokana na kipande kinachomuonesha msanii huyo pamoja na madansa wake wakiwa wamevalia mavazi ya maaskofu na watawa wa kikatoliki.

Kulingana na msemaji wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Charles Twiine, video hiyo imeibua ukakasi na hisia za dharau juu ya dini , hivyo vyombo vyote vya utangazaji na mitandao ya kijamii nchini Uganda vimetakiwa kutorusha video ya wimbo huo hadi pale uongozi wa Fresh Kid utakapo rekebisha sehemu hiyo ya video.

“Nimeangalia video ya wimbo wa Fresh Kid akiwa amevaa kama Askofu huku wacheza densi wake wakivaa kama watawa wa Kikatoliki, nimechukizwa sana na mameneja wake. Video kama hizo hazipaswi kamwe kuchezwa kwenye vyombo vya habari,” alisema.

Video mpya ya Fresh Kid “Maziima” ni kati ya video zinazovuma (trend) sana kwenye mtandao wa YouTube Uganda ambapo kwa sasa inakamata nafasi ya tatu kwenye trending tab.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke