Wasanii wa muziki nchini Uganda Vinka na Irene Ntale walikuwa marafiki wakubwa kipindi cha nyuma.
Vinka Alikuwa wakala wa kuratibu maombi ya shows za Ntale chini lebo ya muziki ya Swangz Avenue, lakini Vinka alipoamua kufanya muziki, uhusiano wao uliingiwa na ukungu. Jambo hilo lilimlazimu Ntale kugura lebo hiyo na tangu wakati huo kumekuwa na chuki baina ya wasanii hao wawili.
Kulingana na Vinka, walifanya wimbo pamoja uitwao “Stylo” kabla ya Ntale kuondoka kwenye lebo ya swangz avenue, lakini kipindi wanafanya video ya wimbo huo, Ntale aliondoka location bila kutoa maelezo yeyote, huku akimuacha Vinka njia panda.
“Nililia siku hiyo. Kulikuwa na mvutano siku hiyo. Sijui ni nini kilisababisha. Nilihisi kusalitiwa na rafiki yangu mkubwa. Siku hiyo nilisubiri maelezo yake lakini hakuzungumza,” Vinka alisema kwenye mahojiano.
Hitmaker huyo “Thank God” amesema kuwa hajawahi fahamu chanzo cha Ntale kuondoka wakiwa location wakishoot video ya wimbo wao.
“Niliapa kutomuuliza au kuwasiliana naye kwa sababu nilihisi yeye ndiye atanitafuta anielezee kilichochea uhasama wetu,” aliongeza.
Maisha ya Irene Ntale kimuziki hayajawa kuwa sawa tangu alipoachana na lebo ya Swangz Avenue mwishoni mwaka wa 2017 baada ya kuachia nyimbo kali. Ntale alipoteza akaunti zake za mitandao ya kijamii kwa uongozi wake wa zamani na hili lilimkatisha tamaa mrembo huyo kuendelea na muziki wake.