Mwanamuziki wa Swangz Avenue Vinka amekanusha madai yanayosambaa mtandaoni kuwa alifanyiwa upasuaji kwa ajili ya kuongeza makalio yake.
Katika moja ya onesho lake huko nchini Uganda Vinka amewaambia mashabiki zake kuwa amepata mabadiliko makubwa kwenye mwili wake mara baada ya kujifungua mtoto wake mwishoni mwa wa 2021 jambo analodai limempelekea kuanza mazoezi ya kuweka mwili wake sawa.
Utakumbuka kipindi vinka anaanza muziki miaka kadhaa iliyopita alikuwa na mwili mdogo kiasi cha watu kuanza kumfananisha na mwanaume lakini katika siku za hivi karibuni amebadilika kimuonekano jambo ambalo limezua maswali mengi miongoni mwa mashabiki zake wengi wakihoji huenda amefanyiwa surgery kuongeza baadhi ya viungo vya mwili wake.