You are currently viewing VINKA AKANUSHA KUWA KWENYE BIFU NA AZAWI

VINKA AKANUSHA KUWA KWENYE BIFU NA AZAWI

Msanii wa Swangz Avenue Vinka amekanusha madai ya kuwa kwenye ugomvi na msanii mwenzake Azawi.

Katika mahojiano yake hivi karibuni vinka amesema madai hayo hayana msingi wowote kwa kuwa yanachochewa na baadhi ya watu wasiokuwa shughuli ya kufanya maishani.

Hitmaker huyo wa ngoma ya “One Bite” amesema kuwa kama kweli angekuwa na ugomvi na azawi angemuunga mkono kwenye harakati zake za kutangaza onesho lake litakalofanyika hivi karibuni.

Hata hivyo amesema yeye na Azawi ni marafiki wakubwa hivyo wameelekeza nguvu zao zote kwenye suala la kuupeleka muziki wa uganda kimataifa.

Kauli ya Vinka imekuja mara baada ya uvumi kusambaa mtandaoni kuwa ana bifu na Azawi licha ya kwamba wote wamesainiwa kwenye lebo moja ya muziki.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke