Mwanamuziki wa Swangz Avenue Vinka amekanusha madai yanayotembea mtandaoni kuwa alificha uja uzito wake kwa umma mwaka wa 2021.
Katika mahojiano yake hivi karibuni, Vinka amesisitiza kwamba alifanya performances kwenye sherehe za harusi hadi pale alipokaribia kujifungua huku akisema kwamba alikuwa pia akichapisha picha kwenye mitandao ya kijamii akiwa mjamzito.
Hitmaker huyo wa Thank God amesema baada ya kujifungua ilimchukua mwezi mmoja kurudi kuendeleza harakati zake za kuwapa mashabiki zake burudani kwani kuna watu wengi walimpa mialiko ya kutumbuiza kwenye sherehe zao za harusi.
Vinka alibarikiwa na mtoto wake wa kike mwaka 2021 jambo lilowaacha mashabiki zake na mshangao kwani walikuja wakajua alikuwa mja mzito baada ya kujifungua.