You are currently viewing VINKA ATIA SAINI MKATABA MPYA NA LEBO YA SWANGZ AVENUE

VINKA ATIA SAINI MKATABA MPYA NA LEBO YA SWANGZ AVENUE

Mwanamuziki kutoka Uganda Vinka ametia saini mktaba mpya na lebo ya muziki ya Swangz Avenue ikiwa ni mwaka mmoja umepita tangu msanii mwenzake Winnie Nwagi aongeze mkataba wake na lebo hiyo.

Vinka ameweka wazi habari hiyo njema kwa mashabiki zake kupitia ukurasa wake wa Instagram akitia wino mkataba wake wa miaka 5 na lebo hiyo kwenye hafla iliyoshuhudiwa na Afisa mkuu mtendaji wa Swangz Avenue Julius Kyazze pamoja na wakili wake Joel Plus.

Kulingana na Swangz Avenue Vinka bado ni msanii wa Sony music Africa ambaye ana mkataba mrefu nao ila swangz avenue itabaki kuwa uongozi wake kwa niaba ya Sony music.

Lakini pia lebo hiyo imekanusha taarifa za kuwatema wasanii wake wakongwe baada ya kuwasaini wasanii wapya kama Zafarah na Azawi.

Swangz avenue imekuwa ikisimamia muziki wa Vinka tangu mwaka wa 2016 na mwaka wa 2018 Vinka alisaini mkataba na sony music.

Utakumbuka mpaka sasa Swangz Avenue ina jumla ya wasanii 4 ambao ni Winnie Nwagi, Azawi, Vinka na Zafaran ambaye alisainiwa majuzi na lebo hiyo.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke