You are currently viewing VINKA AZUA GUMZO MTANDAONI BAADA YA KUSAHAU JINA LA WIMBO WAKE AKIWA LIVE NBS TV

VINKA AZUA GUMZO MTANDAONI BAADA YA KUSAHAU JINA LA WIMBO WAKE AKIWA LIVE NBS TV

Baada ya kusainiwa na lebo ya sony Entertainment Group msanii kutoka nchini Uganda Vinka alipunguza idadi ya nyimbo alizokuwa anatoa kwa  mashabiki zake.

Msanii huyo wa Swangz Avenue aliachia nyimbo tatu mwaka wa 2021 ambazo ni Thank God, Loving akiwa amemshirikisha Roberto na Kimuli Kyange aliyoshirikishwa na Mudra.

Sasa akiwa kwenye mahojiano na NBS TV Vinka aliwashangaza wadau wa muziki nchini Uganda baada kutaja majina ya nyimbo zake mbili na akapata kigugumizi kutaja jina la wimbo wake wa tatu ambao ni Loving.

Jambo hilo lilimfanya Vinka kuwaomba mashabiki zake msamaha kwa kitendo cha kusahau jina la wimbo wake wa tatu akiwa hewani baada ya mtangazaji wa kituo cha runinga cha NBS kumkumbusha jina la wimbo huo.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke