You are currently viewing VIVIAN AWAPA SOMO WASANII WA KIKE NCHINI KENYA

VIVIAN AWAPA SOMO WASANII WA KIKE NCHINI KENYA

Msanii nyota nchini Vivian amewapa somo mastaa wa kike kwa kuwataka wajitume ili kujiletea maendeleo kwa kuwa muda wa kutumiwa kingono na wanaume umepita.

Akizungumza na Mungai Eve, Vivian amesema kuwa baadhi ya wasanii wamekuwa wakijiweka nyuma na wakati mwingine kukubali kutumiwa kingono ili watoke wakati uwezo wanao.

Vivian ambaye anafanya vizuri na wimbo wake uitwao Chachisha aliomshirikisha Sosuun amesema dhana ya mwanamke shujaa kwake ni yule anayepambana kufanikisha kila kitu huku akisisitiza kwamba mwanamke anaweza kuwa kiongozi, mwalimu au kufanya kazi yoyote iwapo akidhamiria kupambana.

Hata hivyo amewataka wanawake kuondoa dhana ya kuwezeshwa na badala yake wapambane kutunza uanamke wao.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke