Msanii wa kike nchini Uganda Vivian Tendo amekanusha tuhuma za kuwa kwenye mpango wa kufunga ndoa ya siri na bosi wa Wakiso Giants Musa Atagenda.
Katika mahojiano yake ya hivi karibuni Tendo amesema hana uhusiano wowote wa kimapenzi na Musa Atagenda kama inavyodaiwa mitandaoni ambapo ameenda mbali zaidi na kupuzilia mbali mipango ya kuhalalisha mahusiano yao ya kimapenzi.
Hitmaker huyo wa ngoma ya “Timango” amesema hana mpango wa kuingia kwenye ndoa hivi karibuni kwani kwa sasa ameelekeza nguvu zake kwenye suala la kuupeleka muziki kimataifa.
Kauli ya Vivian Tendo imekuja mara baada ya walimwengu kuhoji kuwa huenda mrembo huyo anatoka kimapenzi na mfanyibiashara huyo kufuatia kuonekana pamoja kwenye moja ya video iliyokuwa ikisambaa mitandaoni ikiwaonyesha wakiwatakia mashabiki zao mfungo mwema wa mwezi mtukufu wa Ramadhan.