Mkali wa Dancehall mwenye umaarufu mkubwa duniani Vybz Kartel ambaye kwa sasa anaendelea kusotea gerezani, amemposa mrembo Mturuki Sidem Ozturk.
Kwa mujibu wa Radio ya Nation Wide, posa hilo lilifanyika wakati wa ziara iliyoidhinishwa gerezani humo, ambapo Vybz Kartel anatumikia kifungo cha maisha jela kwa mauaji ya Clive “Lizard” Williams.
Sidem Ozturk ambaye ameajiriwa huko London, Uingereza kama mfanyakazi wa kijamii, amekatiza taaluma yake na kuhamia Kingston, Jamaica ili kuwa karibu na nyota huyo wa Dancehall.
Licha ya changamoto wanazokabiliana nazo kutokana na Kartel kulala nyuma ya nyondo, Ozturk hajakata tamaa katika penzi lao.