Mwanamuziki wa Dancehall nchini Uganda Vyper Ranking amedai kwamba ni sio jambo la kingwana kwa wasanii kuanika mizozo ya familia zao kwenye mitandao ya kijamii.
Katika mahojiano yake ta hivi karibuni msanii huyo wa lebo ya muziki ya Bantu Africa Entertainment amesema vitendo vya wasanii kuanika mitandaoni migogoro yao vitakuja kuwaathiri watoto wao siku za usoni huku akiwataka wasanii wote ambao wana skendo za baby mama au baby daddy zao watatue migogoro yao nje ya mitandao kwani inaleta taswira mbaya kwa jamii.
Kauli ya Vyper Ranking imekuja mara baada ya taarifa za mastaa kuwa kwenye mzozo na watu waliozaa nao kwenye mahusiano yao zamani kushika headlines kwenye mitandao ya kijamii nchini Uganda ikiwemo ya msanii Geosteady na Baby Mama wake Prima Kadarsha