Waendesha Mashtaka kwenye Kesi ya R. Kelly wamemtaka Jaji amhukumu mwimbaji huyo kutoka Marekani kifungo cha zaidi ya miaka 25 Gerezani.
Hii ni baada ya mwezi Septemba kukutwa na hatia ya makosa 9 yanayohusiana na unyanyasaji wa kingono kwa Wanawake na mabinti wenye umri mdogo.
Juni 8 mjini New York, Jopo la Waendesha Mashtaka wa Serikali lilimwambia Jaji kwamba R. Kelly amekimbia hukumu kwa takribani miaka 30, na sasa lazima aende Jela.
R. Kelly amepanga kukata rufaa juu ya maamuzi hayo, na inatakiwa afanye haraka kabla ya Juni 29 mwaka huu kwani ndio siku ya kutolewa hukumu.