Wahisani wameridhia ombi la kumsaidia msanii kutoka Uganda Ronald Alimpa aliyehusika kwenye ajali mbaya barabarani Septemba 29 mwaka huu.
Kwa mujibu wa picha zinazosambaa mtandaoni, Hitmaker huyo wa “Seen Don” anaendelea kupokea msaada wa kifedha na mahitaji mengine ya msingi kutoka kwa wasanii wenzake, mashabiki pamoja na marafiki huku akiwa anauguza majeraha mabaya kwenye hospitali moja jijini Kampala.
Hatua hii imekuja siku mbili baada ya msanii huyo kupitia video iliyosambaa mtandaoni kuwaomba wahisani kuchangisha fedha za kugharamia matibabu yake.