You are currently viewing WAHU AKOSHWA NA SHABIKI YAKE MLEMAVU,ACHANGISHA SHILLINGI 180,000 KUMSAIDIA

WAHU AKOSHWA NA SHABIKI YAKE MLEMAVU,ACHANGISHA SHILLINGI 180,000 KUMSAIDIA

Msanii wa muziki nchini Wahu Kagwi amefanikiwa kuchangisha takriban shillingi elfu 180 kwa ajili ya shabiki yake mmoja anayefahamika kama Eunice.

Eunice ambaye ana changamoto ya ulemavu alikuwa anahitaji kiti cha magurudumu ambacho kinatumia umeme kufanikisha matembezi yake.

Wahu alivutiwa na Shabiki huyo aliposhiriki shindano la tiktok la wimbo wake wa back it up, wimbo ambao uliuachia mwezi oktoba mwaka huu akiwa amemshirikisha Nameless.

Baada ya kuuguswa na ukarimu wa mashabiki zake Wahu kupitia ukurasa wake wa Instagram alitangaza kusitisha mchango huo baada ya kufikisha shillingi elfu 180 ambapo ametumia fursa hiyo kuwashukuru mashabiki zake kwa upendo ambao walimuonyesha Eunice ambaye anaishi na changamoto ya ulemavu.

Ikumbukwe Eunice pamoja washirika na wenzake kwenye challange ya wimbo Back It Up katika mtandao wa Tiktok walialikwa kwenye tamasha la Oktoba Fest la Wahu na Nameless na ndipo Wahu alipata wasaa mzuri wa kunzungumza na Eunice ambapo alifunguka mengi yanayomsibu.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke