You are currently viewing WAHU KAGWI ALAMBA SHAVU LA KUWA BALOZI WA MORTEIN DOOM

WAHU KAGWI ALAMBA SHAVU LA KUWA BALOZI WA MORTEIN DOOM

Staa wa muziki nchini Wahu Kagwi amelapa dili nono la kuwa balozi wa Bidhaa za kuua mbu, Mortein Doom.

Wahu ameshare habari hiyo njema kwa mashabiki zake kupitia ukurasa wake wa instagram akieleza kwamba ana furaha kujiunga na familia ya Mortein Doom kwenye kampeini yao ya kukumaliza malaria iliyopewa jina la “Pambana na Kutokomeza Malaria.”

“Katika nchi yetu ikija kwenye masuala ya Afya katika maeneo mengi, wanawake na akina mama ni mawakala wa mabadiliko na nguvu inayojenga maisha bora kwa familia, na jamii kwa ujumla. Nina furaha sana kufanya kazi na Mortein inapoendelea kuhakikisha Kenya inatokomeza kabisa malaria,” wahu alisema.

Kampuni mama ya Mortein, Reckitt imesema uteuzi wa Wahu kuwa balozi wa bidhaa za Mortein doom unalenga kutoa elimu kwa umma juu ya hatua za kuzuia Malaria huku ikithibitisha kuwa ugonjwa huo hatari pia unaweza kutibika na kutokomezwa.

“Muungano huu unalenga kuhimiza ushirikiano kati ya Mortein na Wahu ili kujenga uelewa kuhusu tishio la mara kwa mara la malaria nchini Kenya na dhamira yetu mpya ya kutokomeza ugonjwa huo,” alisema Meneja wa Reckitt Kenya Asif Hashimi.

Kwa mafanikio hayo, Wahu atatakiwa kutangaza na kuwashawishi wa kenya wazinunue bidhaa za Mortein doom kupitia mitandao yake ya kijamii kupambana na Malaria.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke