You are currently viewing Wahu na Nameless waweka wazi jinsia ya mtoto wao

Wahu na Nameless waweka wazi jinsia ya mtoto wao

Staa wa muziki nchini Wahu ameweka wazi jinsia ya mtoto wake wa tatu ambaye atazaliwa hivi karibuni.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram amechapisha video ya hafla ya utambulisho wa jinsia ya mtoto wao na kusindikiza na maneno yanayosomeka “BabaGalz Chairman honored, excited and ready for Duty!

Ujumbe huo umetafsiri moja kwa moja na watumiaji wa mitandao ya kijamii kuwa Wahu na mume wake Nameless wanatarajia kumpata mtoto wa kike.

Hata hivyo mashabiki na mastaa mbali mbali wamewapongeza wawili hao kwa hatua hiyo wakati huu wapo mbioni kumkaribisha mwanafamilia mwingine.

Utakumbuka juzi kati taarifa zilisambaa mtandaoni zikidai kuwa huenda Wahu alijifungua kwa siri kutokana na jumbe alizokuwa anachapisha kwenye mtandao wake wa Instagram.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke