Kundi la muziki wa hiphop nchini Wakadinali limeachia rasmi album yao mpya iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na mashabiki wao.
Album hiyo iitwayo NDANI YA COCKPIT 3 ina jumla ya ngoma 15 za moto huku wakiwa wamewashirikisha wasanii kama Khaligraph Jones, Wangechi, Kitu Sewer, Kalahari, McGijo na wengine kibao.
NDANI YA COCKPIT 3 ni muendelezo wa Album yao ya mwaka 2017-18 “Ndani ya Cockpit 1 & 2” iliyokuwa na jumla ya singles 9 na 13 mtawalia.
Hii ni Album yao ya nne baada ya “Victims of Madness” ya mwaka wa 2020 na inapatikana ‘Exclusive’ kupitia mitandao yote ya kukisikiliza na kupakua muziki duniani ikiwemo Boomplay,Spotify na Apple Music.
Wakadinali ni kundi la Hiphop kutoka nchini Kenya linaloundwa na wasanii watatu ambao ni Scar, Domani Munga, pamoja na Sewersydaa.