You are currently viewing WALTER CHILAMBO AACHIA RASMI ALBUM YAKE MPYA

WALTER CHILAMBO AACHIA RASMI ALBUM YAKE MPYA

Mwimbaji nyota wa muziki wa Injili nchini Tanzania Walter Chilambo ameachia rasmi album yake mpya iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na mashabiki zake.

Album  hiyo inayokwenda kwa jina la “Ushuhuda”  ina  jumla ya nyimbo 10 za moto, imesheheni nyimbo zenye maudhui tofauti tofauti zitakazogusa maisha yako kwa namna ya kipekee kabisa.

Kwenye album hiyo mpya kutoka kwa Walter Chilambo ambayo inapatikana Boomplay ina nyimbo kama, Unafaa, Nitakase, Busara, Mapenzi ya Milele, Ushuhuda, Asante Baba, Ananipenda, For Your Love, Yule Yule na Messiah.

Hii ni album ya pili kutoka kwa Walter Chilambo baada ya album yake “Thank you Lord” aliyoitoa mwaka 2021.

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. He host an Entertainment show at North Rift Radio 104.5 FM & 104.9 FM called "Interact", that usually runs every Monday to Friday from 1 PM - 4 PM. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke