Mwanamuziki kuoka Marekani Beyonce amejikuta kwenye kiti cha moto kufuatia kutumia neno “Spazzin” kwenye wimbo wake Heated unaopatikana kwenye album yake Renaissance aliyoiachia hivi karibuni
Baadhi ya wanaharakati kwenye mitandao ya kijamii wamehoji juu ya mwimbaji huyo kutumia neno hilo ambalo hutumika kuwadhihaki watu wenye ulemavu wa akili.
Kufuatia tuhuma hizo Beyonce ameahidi kufuta maneno hayo kwenye wimbo huo japo hajaomba radhi mpaka sasa.
Si Beyonce tu aliyewahi kusakamwa kwa kutumia neno hilo ila hata mwimbaji Lizzo alilazimika kubadili mstari kwenye wimbo wake Grrls baada ya kutumia neno hilo
Pamoja na ahadi hiyo ya kubadili maneno hayo kwenye wimbo wake wanaharakati wanataka Beyonce aombe radhi kwa uma kama alivyofanya Lizzo.