You are currently viewing WANAHARAKATI RWANDA WAPINGA TAMASHA LA KOFFI OLOMIDE

WANAHARAKATI RWANDA WAPINGA TAMASHA LA KOFFI OLOMIDE

Wanaharakati wa haki za wanawake nchini Rwanda wamelipinga tamasha la mkongwe wa Rhumba wa Congo, Koffi Olomide kwa tuhuma za ubakaji na unyanyasaji wa kingono anazokabiliwa nazo katika Mahakama za Ufaransa.

Mwezi huu wa Desemba, Mahakama ya Paris nchini Ufaransa itatoa uamuzi wa rufaa iliyoombwa kwa mashtaka dhidi ya Le Grand Mopao Mokonzi ambaye alipatikana na hatia ya kuwanyanyasa kijinsi wanenguaji wake wanne wa zamani.

Juliet Karitanyi, mwanaharakati mjini Kigali, Rwanda anasema kumruhusu Koffi kutumbuiza nchini Rwanda itakuwa ni kutoheshimu waathiriwa wa unyanyasaji wa kingono.

Hata hivyo, baadhi ya watetezi wa Mopao Mokonzi kwenye mitandao ya kijamii wanasema hakuna msingi wa kisheria wa kumzuia kutumbuiza nchini Rwanda

Elim Robert

Robert Elim is an Editor with high interest and knowledge in the entertainment space, an industry he has been actively part of since childhood. Leads to breaking stories are welcome at elimrobert@gmail.com & contact@urbanspice.co.ke