Mwanamuziki kutoka nchini Kenya Jovial amedai kwamba wanaume wengi siku hizi wanaogopa kuingia kwenye ndoa.
Kupitia instastory yake ameandika ujumbe mrefu akisema kuwa wanaume wengi nchini wana afadhilisha kuzaa kwanza na wapenzi wao kabla ya kuhalalisha mahusiano yao kwa njia ya harusi.
Msanii huyo anahoji kuwa wanaume wa karne hii hawaaminiki katika kuingia kwenye mahusiano ya kudumu kwani wengi wao wana kasumba ya kukatisha uchumba ghafla bila ya kutoa taarifa kwa wanawake wao.
Jovial amesema kitendo cha watu kukimbia ndoa kumpelekea maduka ya kuuza mavazi ya harusi kupungua sana nchini ikilinganishwa na mataifa ya nje, jambo ambalo anadai limewakosha wafanyibiashara fursa ya kuingiza kipato.
Hata hivyo amedokeza mpango wa kutunga wimbo maalum kwa ajili ya wanaume wasiopenda masuala ya kufunga ndoa katika jamii.